Soy Power Capsule
Viungo:
Semen Glycine, Radix Paeoniae Alba Extractum, Ganoderma, Soy Isoflavones
.
Kazi Na Faida Zake
- Kuzuia kudorora kwa ufanyaji kazi wa ovari
- Kupunguza kupungua uzito wa mifupa, kuzuia osteoporosis, hasa wakati na baada ya kukoma hedhi
- Kuzuia kansa ya maziwa
- Kuzuia arteriosclerosis na magonjwa ya mishipa ya damu
- Kuboresha ufanyaji kazi wa ubongo, kuboresha kumbukumbu na kuzuia dementia
- Kuchelewesha kuzeeka, kuboresha ngozi na kuifanya laini, inayonyumbuka.
Yafaa Kwa:
- Wanawake wenye msongo wa mawazo kabla ya kukoma hedhi
- Wanawake wenye matatizo ya kukoma hedhi
- Wanawake wenye homoni ambazo hazina uwiano (unbalanced hormones), hasa kupungua kwa estrogen
- Wanawake wenye mifupa myepesi au wenye osteoporosis
- Wanawake wagumba uliotokana na kiwango cha estrogen
- Wanawake wanaokosa usingizi au wenye wasiwasi
- Wanawake wanaotaka kuboresha hali ya kufanya mapenzi
Maelezo Muhimu:
Shughuli Zinazolingana na Za Estrogen na Shughuli Tofauti na za Estrogen (Estrogenic and Anti-Estrogenic Activities):
Isoflavones za soy zinaeleweka kuwa na tabia kwa mbali za estrogen, yaani zinafanya kazi kama homoni ya estrogen. Estrogens ni molekuli za kutoa ishara ambazo zinatoa matokeo kwa kushikana na vipokezi vya estrogen (estrogen receptors) ndani ya seli. Muundo huu mkubwa wa vipokezi vya estrogen unatendana na DNA na kubadilisha mwonekano wa vinasaba vya vipokezi vya estrogen. Vipokezi vya estrogen vinapatikana katika tishu zingine nyingi zaidi ya zile zinazohusika na uzazi, kama kwenye mifupa, ini, moyo, na ubongo. Isoflavones za soy na phytoestrogens nyingine zina uwezo wa kunatana na vipokezi vya estrogen, na kuonyesha tabia za estrogen yenyewe katika baadhi ya tishu huku zikizuia matokeo ya estrogen katika tishu nyingine. Wanasayansi wanapenda kuona tabia hii ya kuweza kuchagua tishu ya phytoestrogens kwa sababu uwezo wa kuzuia matokeo ya estrogen katika viungo vya uzazi ungeweza kusaidia kuondoa uwezekano wa kutokea kwa kansa zinazohusishwa na homoni (maziwa, njia ya mkojo, na tezi dume), wakati kuwepo na matokeo ya shughuli za estrogen katika tishu nyingine kungeweza kusaidia kudumisha ubora wa mifupa na kuboresha viwango vya cholesterol katika damu.
Antioxidants:
Isoflavones za soy zina tabia ya antioxidants ya kulinda mishipa ya moyo dhidi ya oksijeni inayoharibu cholesterol ya LDL (Cholesterol mbaya). LDL iliyoathiriwa na oksijeni hujikusanya ndani ya arteri kama vijifungu vya mafuta ambavyo baadaye huzuia mtiririko wa damu, na kusababisha atherosclerosis. Soy Power Capsule huzuia kukua kwa seli ambazo husababisha uzibaji huu wa arteri. Arteri ambazo zimeharibiwa na atherosclerosis kwa kawaida husababisha kuziba kwa damu. Hii huweza kupelekea tatizo la shinikizo la damu (heart attack) kama damu hii iliyoganda itaelekea kwenye moyo, au kiharusi kama italekea kwenye ubongo.
Kuzuia Kansa Ya maziwa:
Kwa kuwa ni mfano wa estrogen dhaifu, isoflavones zinaweza kuleta ushindani kwenye maeneo ya vipokezi vya estrogen, kuizuia estrogen asilia yenye nguvu inayotengenezwa na mwili isifanye kazi yake kamili. Kwa kuwa uwingi wa homoni ya estrogen katika damu ni jambo ambalo limedhihirika kuwa ni chanzo cha kansa ya maziwa, aina hizi za estrogen dhaifu zinaweza kusaidia kuleta kinga dhidi ya ugonjwa huo. Ikiwa inasaidiana na Ganoderma na majani mengine, Soy Power Capsule inaweza kuzuia kansa zinahusiana na estrogen kama kansa ya maziwa.
Kuimarisha Mifupa:
Soy Power Capsule inaweza kufanya kazi ya kulinda na kuweka mifupa kuwa yenye nguvu na afya. Inaweza kuongeza uwingi wa madini katika mifupa na uzito wa mifupa, na vile vile kuanzisha ujengwaji wa mifupa. Kwa hiyo Soy Power capsule inasaidia kuzuia na kurekebisha tatizo la osteoporosis ( mifupa kupungua ujazo, kuwa milaini na kuvunjika kwa urahisi).
<<<<< MWANZO